Posts

Showing posts from May, 2017

JINSI YA KUPATA MCHUMBA SAHIHI

Moja ya mambo ya msingi ambayo kila kijana anahitaji ni Ndoa ya Kudumu ukiacha ongezeko la kufeli kwa ndoa nyingi. Wakati huohuo moja ya uamuzi (wa maana sana katika maisha ya binadamu ni kuamua nani atakuwa mume wako au mke wako na huu uamuzi ndiyo utakufanya uweze kuishi maisha ya namna gani katika ndoa yako na pia kuathiri kabisa mfumo wa maisha yako kuwa raha au kuwa karaha Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao. Huu ni ujinga muhusika mara nyingi ni wewe kwani asilimia 99 ni jinsi ulivyompata huyo mtu ambaye amesababisha ndoa yako au uhusiano kuvunjika. Mtu anayestahili kupewa lawama zote ni wewe. Kama hujaolewa au ndio upo kwenye process za kuolewa au kuoa,Fahamu kwamba hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha hapa duniani. Unahitaji kutumia akili zako zote, maombi yako yote, uw...

KWANINI UKATE TAMAA??

Kuna baadhi ya wanandoa tena kwa machozi wamekuwa wakilalamika kwamba partners wao hawawezi kuongea nao tena! Hawezi kushirikisha kitu chochote ingawa wanaishi nyumba moja, wanakula chakula kimoja, wanalala kitanda kimoja na wengine wana watoto pamoja. Wamejikuta ndoto zao zinayeyuka na ladha ya ndoa na maisha kwa ujumla imekuwa chungu. Kama unapitia upweke wa aina hii na kujikuta unajuta kuishi na mume au mke wa aina hii bado kuna matumaini na kuna nafasi kubwa ya kuweza kurudisha kwenye mstari, jaribu kufanya yafuatayo. 1;TEMBEA KATIKA ROHO. Ndoa si two-way street kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke au kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume bali ni three way street kati ya mke, mume na Mungu. Tunapotembea katika Roho, Mungu anamwaga upendo wa kutosha kati ya mke na mume. Breakdown yoyote kati ya mke au mume na Mungu huweza kusababisha wanandoa kuanza kuvurugana ndiyo maana wanandoa ambao hofu ya Mungu, kutembea katika Roho ni Nambari one basi wamebarikiwa kw...

USIJARIBU KUMFANANISHA NA WENGINE.

Kuna wakati huwa inashangaza sana ukisikia yale wanandoa wanafanya au wanataka yafanyike katika ndoa zao. Kama ni mwanamke basi una marafiki wanawake wenzako ambao waume zao inawezekana wana pesa nyingi kuliko mumeo, wamesoma kuliko mumeo, wana mali kuliko mumeo, wana akili kuliko mumeo, wanakuwa na muda zaidi na familia zao kuliko mumeo, wakivaa wanapendeza kuliko mumeo na pia wanabembeleza wake zao kuliko mumeo, au wana tabia njema kuliko mumeo au kama wewe ni mwanaume nawe una marafiki wa kiume ambao wake zao wapo hivyo. Je, ni mara ngapi umemlalamikia mumeo au mkeo kwa kumlinganisha na wanaume wengine au wanawake wengine? Inawezekana umemlalamikia mumeo au mkeo kwamba “Mwenzako jerry amepunguza uzito wewe umebaki umenenepeana kama kitimoto kwa nini? “Mwenzako George amenunua gari wewe nini kinakushida , wewe ni mwanaume gani?” “Mwenzako mama Noel kila siku ukienda kwake nyumba safi wewe inakuwaje chafu namna hii” Kama ni wewe utajisikiaje? Hapa msipotoana ngeu au k...

KUACHANA SI SULUHISHO.

Wewe ambaye umeoa au kuolewa na upo unafikiria kuachana na mwenzi wako. Fikiria upya uamuzi wako. Fikiria hao watoto mlionao, Fikiria nyakati zote nzuri mlizokuwa nazo pamoja kama mke na mume, Fikiria sehemu tofauti ambazo mlitembelea pamoja, marafiki wazuri mliokuwa nao wote wawili kama mke na mume. Iepuke talaka kwa gharama zote, sababu zinazokufanya uamue kuachana na huyo mume wako au mke wako zinaweza kuwa ndizo zitakazokuwa sababu mara nyingine tena mbele ya safari kama utaamua kuoa au kuolewa tena. Sasa unaachana na Jimmy kwa kuwa umechoka na tabia zake za kulewa sana pombe, au kukutaka sex mara nne kwa siku na next time unaweza kujikuta unaachana na John kwa kuwa anakupiga mingumi usiku kucha na yeye sex kwa mwaka mara moja. Inawezekana unataka kuachana na mary kwa sababu ni msumbufu na anakusema hata kwa vitu vidogo, hata hivyo unaweza kujikuta unaacha na Joyce baadae kwa sababu si mwaminifu katika fedha. Sasa utaishia wapi na hiyo project ya kuachana na kil...

MAMBO HUBADILIKA MKISHAOANA NA KUANZA KUISHI PAMOJA

Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja. Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanz a kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena. Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja. Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa. Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenz...

NI MAKOSA KUMPA MCHUMBA HUDUMA ZA MKE/MUME

Kawaida huwezi kumpa kila mwanaume huduma za mume wakati bado ni mchumba tu. Vijana wengi leo wanapochumbiana au kutafuta urafiki wa kawaida kati ya kaka na dada (dating) wengi hawajajua kwamba hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa na ni kama usaili tu wa kumpata mtu wa kuoana naye. Ndoa na uchumba (girlfriend/boyfriend) ni vitu viwili tofauti kabisa uchumba huhusisha kumfahamu mwenzako kama anafaa kuwa mke au mume na ndoa ni agano na kumkubali mtu kuishi naye “ hadi kifo. Hata siku moja uchumba si ndoa na ndoa si uchumba. Ukimpa mchumba haki za mume au mke siku mkiachana na huo uchumba (kitu ambacho ni kawaida kama ukiona candidate uliyenae katika uchumba hawezi kwa excellent material ya ndoa) utaumizwa zaidi hasa mwanamke kwani mwanaume anaweza kumpata binti mwingine jioni yake au usiku huohuo na akaendelea na maisha. Kinachoshangaza pia ni kwamba hata relationship inapovunjika mara nyingi mwanaume huumia kidogo kwa kuwa mwanaume siku zote anapoingia kwenye mapenzi hu...

MWANAMKE JIFUNZE HAYA

1. Ukiwa Kama mwanamke, pale panapotokea maudhi dhidi ya mpenzi wako, nyamaza kimya, ukimya wa mwanamke humsumbua akili mwanaume. Atahisi kuna jambo fulani kichwani mwako na kama anabusara atatafuta njia ya kusuruhisha. Usiwe mtu wa tit-for-tat. 2. Kama atakutumia ujumbe wa maudhi katika simu, usimjibu kwa maneno ya kuudhi pia. Muandikie "Samahani" au "Asante sana." 3. Hakuna mwanaume anapenda mwanamke anaemrudishia maneno, kama wewe ni mke uliye na busara, funga mdomo wako. Pale atakapokuwa ametulia ongea nae mmalize mgogoro. 4 Usilingie uzuri wako. Hujawaona wanawake wazuri wengi tu bado wako single, lakini wanaishia kuwa wezi wa waume za watu na uzuri wao kama wameshushwa toka mbinguni? Tabia yako itakuhifadhi katika moyo wake. 5. Kamwe usimfananishe na EX wako au mwanaume mwingine, huwezi jua huyo mwanaume nae ana mapungufu gani katika mahusiano yake. Binadamu hatuko 'perfect' 6. Usiwe wa kupokea tu, mnunulie chochote, haijalishi kama...

USITISHWE NA HISTORIA YAKO YA MAHUSIANO

USITISHWE NA HISTORIA... Historia ina athari mbaya kwenye mahusiano. Unaweza kuogopa kuanzisha mahusiano kwa sababu ya mikasa uliyowahi kukutana nayo. Unajikuta ukichukua tahadhari nyingi kupindukia na hata kuapa hutakaa uamini wanaume/wanawake. Ni kama unaamini, "Wanaume/wanawake wote lao moja..." "Wanawake/wanaume wote ni matapeli. Hawafai" Kuumizwa na wasaliti wawili watatu, kunakufanya ufikiri kila mwanaume/mwanamke duniani ni msaliti. Huamini kuwa watu wanaweza kuwa na uhusiano usio na mikasa. Sikusudii kukushauri. Nakumegea sheria ya mahusiano. Tunavutia kinachofanana na sisi. Kwamba huenda kuna kitu fulani unacho [na pengine hukijui] lakini ndicho kinachovutia watu wenye tabia fulani usizozipenda. "Inakuwaje kila nikizama kwenye mahusiano naibuka na matapeli?" "Mbona mwanzoni wanakuwa-ga kama malaika [...] lakini baada ya muda wanakuwa mashetani?" "Kwa nini huwa najikuta naachana na wapenzi kwa mikasa ya kutisha?...

BAADHI YA MAMBO YANAYOSTAWISHA MAHUSIANO NA NDOA.

BAADHI YA MAMBO YANAYOSTAWISHA MAHUSIANO NA NDOA . 1. Kamwe msiweke siri kati yenu, kuwa mahali ambapo umemwambia utakuwepo, msidanganyane. 2. Siku zote mkumbatiane na kum kiss kabla hamjaondoka nyumbani kwenda kwenye mihangaiko. 3. Mwenzako anapoongea, usitumie masikio tu kumsikiliza. Tumia na moyo wako pia. 4. Kamwe msiongelee mambo yaliyopita katika mahusiano yenu, mjikite katika future yenu. Ya kale hayana faida. 5. Siku zote mle pamoja kama kuna uwezekano huo na mlale pamoja kila usiku! 6. Tenga muda wako wa weekend kwa ajili ya familia yako, kuwa karibu na mpenzi wako na wanao kama unao! 7. Kama mko mambo safi sio mbaya mkaenda hata nje ya mji mnaoishi, wawili tu mkafurahia weekend yenu huko sehemu tulivu. Hii inaamsha mapenzi upya. 8. Kama unataka mabishano fanya hivyo kwa busara na kwa hoja, usifanye papara jifunze kunyamaza na kusikiliza. 9. Siku zote jikumbushe kwamba mapenzi ya kweli ni adimu kuyapata, hauwezi kupata mwingine atakaekupenda kama huyo, ...

SIO KUWA MIAKA HII WANAUME WAOAJI HAMNA BALI TABIA YAKO NDIO MCHAWI WAKO

Image
Binti umekaa nyumbani hadi wazazi wako wanapata wasiwasi wanahisi umerogwa, kama ni uzuri unao, kama ni elimu unayo ya kutosha, kama ni dini umeshika na maadili tena mzima wa afya ila ni miaka 30 au zaidi sasa inaenda bado wajipodoa mbele ya baba yako nyumbani hakika inauma, inasikitisha, inakatisha tamaa. Sio kuwa wanaume wote hawataki kuoa ila huenda tabia kati ya zifuatazo unayo na ndio inayokuponza : 👉 VIGEZO VISIVYO NA MSINGI. 🔹 Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana wanaume inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe. 🔹 Binti unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome boy, mrembo wa sura anavaa vizuri awe na hela gari nyumba au kupando cha moto sijui awe na kazi nzur, awe na upendo wa kweli, na mambo mengi kama hayo. 🔹 Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa. Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi. 🔹 kuna...

KWANINI WANAWAKE HUDANGANYA KUFIKA KILELENI?

Kila mmoja amesikia tetesi au fununu kwamba wanawake hudanganya kwamba wamefika kileleni. Ni kweli hili jambo lipo; wanawake wengi wameshawahi kuwafunga kamba wanaume zao zaidi ya mara moja na wengine ni kamchezo kao ka mara kwa mara, hata wewe unayesoma hapa inawezekana usiku ulimdanganya kwamba umefika kileleni kumbe usanii mtupu. Swali la kujiuliza hivi kwa nini wanachukua uamuzi wa kudanganya kwamba wamefika kileleni wakati si kweli? Lazima kutakuwa na sababu za msingi kwani wanawake ni viumbe wanaojua kupenda kuliko wanaume na kama kuna sababu za msingi hii ina maana hawastahili kulaumiwa. Pia tumesikia kwamba mwanaume ukiwa na wallet nzito mwanamke hufika kileleni haraka zaidi tena kwa kelele utadhani ni vuvuzela. Katika dodosa dodosa akina dada wengi na akina mama wengi sababu kubwa zinazopelekea wawadanganye wanaume zao kwamba muziki umejibu kwanza ni kitendo cha kutopenda waume zao wajisikie kuwa discouraged kwani wakati mwingine wao wanawake huwa wanakuwa ...

MME MWENYE BUSARA

Mwanaume mmoja alimuoa msichana aliyekua ni mrembo kweli. Katika kuishi kwao katika maisha ya ndoa, mwanamke alipatwa na ugonjwa wa ngo zi. Taratibu akaanza kupoteza uzuri wake. Ikatokea siku moja mume akasafiri kwenda kufanya kazi sehemu na wakati akirudi akapata ajali mbaya ya gari iliyopelekea awe kipofu. Hata hivyo maisha yao yaliendelea kama kawaida mume akiwa haoni na mke akiwa na ugonjwa mbaya wa ngozi. Siku zilizidi kwenda na ule ugonjwa wa ngozi ukazidi kumshambulia vibaya yule mke, ila mumewe aliendelea kumpenda na maisha ya kupendana yalitamalaki ndani ya mji wao. Ilifika siku yule mwanamke alifariki, kifo cha mkewe kilimhuzunisha sana bwana yule. Walifanya mazishi na baada ya mazishi bwana yule akataka kuhama kabisa mji ule. Ndugu wa bwana yule wakamwambia, umefiwa na mkeo ni nani sasa atakua akikuongoza njia na hali hii wewe huoni? Bwana yule akawajibu, mimi sio kipofu, muda wote huo nilikuwa nikiigiza, kwa sababu mke wangu angejua nauona ubaya wake...

UPENDO WA AJABU..

Wapenzi wawili walipendana sana tangu wakiwa shuleni na waliahidiana siku moja waje kuoana na kujenga familia Baada ya kuhitimu masomo yao kij ana alipata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi. Kabla hajaondoka kijana alisema "sijajaliwa kuwa na maneno mazur sana ila ninachoweza kusema ni kwamba nakupenda sana, na nitakulinda maisha yangu yote" Lakini pia akaomba akawaone wazazi wa binti ili apete kumchumbia. Wakakubaliana na hata walipofika kwa wazazi wala hakukuwa na ugumu wowote wazazi walifurahi kijana akamchumbia binti na kisha akaenda zake masomoni Kijana akiwa masomoni waliendelea kuwasiliana kupitia email na kupigiana simu japo ilikuwa vigumu kuendesha mapenzi yao kupitia simu lakini hakuna aliyefikiria kukata tamaa. Siku moja msichana akiwa ametoka kwenye mizunguko yake kwa bahati mbaya aligongwa na gari na kupoteza fahamu. Alipokuja kuzinduka alijikuta yupo hospitalini huku wazazi wake wakiwa wamekaa pembeni ya kitanda chake. Na akagundua kwam...

YAFAHAMU MAMBO YATAKAYO FANYA MAHUSIANO AU NDOA YAKO KUDUMU

Image
Katika maisha yoyote ya ndoa au mahusiano zipo changamoto mbalimbali zinazo sababisha ndoa au mahusiano mengi kufa. Hata hivyo kufa kwa ndoa nyingi na mahusiano hayo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani . Katika makala hii ya leo ningependa kushiriki pamoja katika kukuletea mambo mbalimbali yanayoweza kufanya ndoa au mahusiano yako yadumu . Mambo hayo ni pamoja na ; 👉 Hofu ya Mungu . Hakuna ndoa yoyote ile iliyoweza kuwa imara na kudumu ikiwa hakuna hofu ya Mungu baina ya wanandoa . Kama ni kijana mwenye lengo la kuingia kwenye ndoa yakupasa kujilidhisha juu ya mchumba uliyenaye kama ni kweli ana hofu ya Mungu . Starehe ya muda mfupi isikufanye ukajisahau na kuingia kwenye ndoa kwa kukurupuka . 👉 Mapenzi ya kweli baina ya wapenzi . Ili uweze kudumu katika ndoa au mahusiano yoyote yale , yakupasa kuwa na mapenzi ya dhani kati ya wewe na mwenzi wako . Kutokuwa na mapenzi ya kweli katika mahusiano hudharisha udanganyifu mk...

MWANAUME AMBAYE SI MUAMINIFU HUYAFANYA HAYA

1. Muda mchache sana huutumia na wewe. Hii huwa tofauti na kipindi cha mwanzo cha mahusiano yanapoanza. Ambapo muda mwingi hupenda kuwa karibu yak. Kukusikia kama si kukuona kabisa. 2. Hana hamu nawe ya kimapenzi tena. Tofauti na mwanzo au ilivyozoeleka katika mahusiano yenu. Kama yeye alikuwa akikuhitaji faragha, basi sasa hata kama ni wewe ndiye unemuhitaji basi atakujibu amechoka. 3.Atakuwa anakukwepa. Atakwepa mawasiliano nawe atakwepa kuonana na wewe atakwepa majukumu yake ya kawaida aliyokuwa anakufanyia siku zote kipindi mnaanza mahusiano 4 Atakuwa mkali tofauti na mwanzo. Hathamini tena kukubembeleza pale atakapoona amezidisha ukali katika sauti yake. Hathamini chozi lako hata ukilia mbele yake. 5. Hasira za haraka zitakuwa juu yake. Hii inatokana na kutafuta ufanye kosa dogo ili akuache mazima hata wakati mwingine si kweli kwamba ulichomtania kitakuwa kimemuudhi kweli 6. Atabadilisha muonekano wake yaani kama ni nywele atabadilisha style na nguo atape...

PENZI LAKO LIMECHUJA, JE UNAJUA CHANZO?

Leo nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja. Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana. Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hayo. Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi alivyo fundi wa 'kuyarudi' ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manj...

TAMBUA UTAMU WA MAPENZI NA JINSI YA KUULINDA KATIKA MAHUSIANO

Kuna sababu za msingi kabisa kuelezea mambo ya kuzingatia ili kutambua vitu vitakavyokufanya ufurahie utamu wa ndoa yako. Kuishi na mke au mume sii kitu rahisi kama ambavyo watu wengi ambao hawako katika ndoa hufikiria. Hivi ni vipengere baadhi tu, wanandoa na wampenzi wanapaswa kuvitambua; Kwanza kabisa ni kwambie kwamba utamu wa mapenzi sii lazima ufanye tendo la ndoa ama ngono, kuna mambo kibao ambayo moyo wa binadamu ukiyakosa huweza kukonda kama muathirika wa magonjwa hatari ya mwili.  #"Upendo kutoka kwa yule umpendae", hili ndilo jambo kubwa la kwanza katika afya ya moyo ulio katika dimbwi la mapenzi. Hakuna kitu kitamu kama kupendwa na ukapenda pia, kitendo hiki hufunga macho yote ya vishawishi vya dunia hii ya kidigitali. Usilazimishe upendo kwa mtu ambae unaonekana kuwa wewe tu ndiye unaye mjali wakati yeye hana habari na wewe. Ndio maana ukitaka kuingia katika ndoa lazima umtafute mtu unayempenda na anayekupenda ili muishi katika maisha yasiyo ...