MME MWENYE BUSARA

Mwanaume mmoja alimuoa msichana aliyekua ni mrembo kweli. Katika kuishi kwao katika maisha ya ndoa, mwanamke alipatwa na ugonjwa wa ngozi. Taratibu akaanza kupoteza uzuri wake.
Ikatokea siku moja mume akasafiri kwenda kufanya kazi sehemu na wakati akirudi akapata ajali mbaya ya gari iliyopelekea awe kipofu. Hata hivyo maisha yao yaliendelea kama kawaida mume akiwa haoni na mke akiwa na ugonjwa mbaya wa ngozi.
Siku zilizidi kwenda na ule ugonjwa wa ngozi ukazidi kumshambulia vibaya yule mke, ila mumewe aliendelea kumpenda na maisha ya kupendana yalitamalaki ndani ya mji wao.
Ilifika siku yule mwanamke alifariki, kifo cha mkewe kilimhuzunisha sana bwana yule. Walifanya mazishi na baada ya mazishi bwana yule akataka kuhama kabisa mji ule.
Ndugu wa bwana yule wakamwambia, umefiwa na mkeo ni nani sasa atakua akikuongoza njia na hali hii wewe huoni?
Bwana yule akawajibu, mimi sio kipofu, muda wote huo nilikuwa nikiigiza, kwa sababu mke wangu angejua nauona ubaya wake uliosababishwa na kuharibika kwa ngozi yake ingemuumiza zaidi na kujiona hana thamani tena kwangu.
Hivyo nilijifanya kipofu ili niitunze furaha yake, alikua ni mke mzuri kweli kwangu.
FUNZO.
Japo kisa hiki ni cha kufikirika (fictional) ila ni vema tujifunze kwamba bora tujifanye vipofu na kupotezea madhaifu ya wapenzi wetu ili tujenge mahusiano ya furaha.
Haijalishi ni mara ngapi meno yanang'ata ulimi wako, ila bado ulimi na meno vipo pamoja mdomoni mwako.
Huo ndio moyo wa KUSAMEHE. Ingawa macho hayaonani ila yote yanaona vitu kwa pamoja, yanafumba na kufumbua pamoja na kulia pamoja. Hiyo ni spirit ya UMOJA.
Mungu atujalie tuwe na spirit ya kusamehe na ya Umoja.
Peke yangu naweza 'kusema' ila pamoja tunaweza 'kuongea'
Peke yangu naweza 'kufurahia' ila kwa pamoja tunaweza 'tukasheherekea'
Huo ndio uzuri wa mahusiano mema, sisi si kitu bila ya mmoja wetu.
Wembe ni mkali lakini haukati mti, na shoka ina nguvu lakini huwezi kunyolea nywele.
Kila mmoja wetu ni wa muhimu kutokana na upekee wake.
acha dharau, muheshimu mtu vyovyote awavyo.
Tuvumiliane why me hivi karibuni ndugu zangu

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPATA MCHUMBA SAHIHI

TAMBUA UTAMU WA MAPENZI NA JINSI YA KUULINDA KATIKA MAHUSIANO

YAFAHAMU MAMBO YATAKAYO FANYA MAHUSIANO AU NDOA YAKO KUDUMU