UPENDO WA AJABU..

Wapenzi wawili walipendana sana tangu wakiwa shuleni na waliahidiana siku moja waje kuoana na kujenga familia
Baada ya kuhitimu masomo yao kijana alipata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi.
Kabla hajaondoka kijana alisema "sijajaliwa kuwa na maneno mazur sana ila ninachoweza kusema ni kwamba nakupenda sana, na nitakulinda maisha yangu yote"
Lakini pia akaomba akawaone wazazi wa binti ili apete kumchumbia.
Wakakubaliana na hata walipofika kwa wazazi wala hakukuwa na ugumu wowote wazazi walifurahi kijana akamchumbia binti na kisha akaenda zake masomoni
Kijana akiwa masomoni waliendelea kuwasiliana kupitia email na kupigiana simu japo ilikuwa vigumu kuendesha mapenzi yao kupitia simu lakini hakuna aliyefikiria kukata tamaa.
Siku moja msichana akiwa ametoka kwenye mizunguko yake kwa bahati mbaya aligongwa na gari na kupoteza fahamu.
Alipokuja kuzinduka alijikuta yupo hospitalini huku wazazi wake wakiwa wamekaa pembeni ya kitanda chake.
Na akagundua kwamba alikuwa ameumia vibaya baada ya kuona mama yake analia.
Na alipotaka kumuuliza ndipo alipogundua kwamba hawezi kutoa sauti zaidi ya midomo kuchezacheza tu.
Daktari akasema "madhara yaliyojitokeza kwenye ubongo yamepelekea kupoteza sauti yake
Hivyo hatokuwa na uwezo wa kuzungumza.
Baadae aliruhusiwa kurudi nyumbani
Akiwa amepoteza kabisa matumaini ya kuja kuolewa na mwanaume aliyempenda kwa kuwa ameshakuwa bubu. Na kwa kutaka kijana asijue kile kilichotokea.
Aliamua kuukatisha uchumba wao kwa kumuandikia barua akisema "sita weza kuendelea kusubiri hivyo endelea na mambo yako na mimi nifanye yangu"
Pete ya uchumba pia akairudisha.
Baada ya hapo kijana alituma mamilioni ya email, akapiga simu mara milioni kasolo lakini hakuna kilichojibiwa
Muda wote huo msichana alikuwa anabaki kulia tu huku akiwa hajui nini cha kufanya.
Baadae wazazi wake waliamua kumuhamisha na kumpeleka mji wa mbali ili walau aweze kusahau na kuirudisha furaha yake.
Akiwa kwenye mazingira mapya/ugenini msichana alijifunza lungha ya ishara (vitendo)na kuanza maisha mapya huku akijiambia mwenyewe kila siku kwamba "ipo siku nitamsahau huyu mwanaume"
Siku moja alikuja rafiki yake na kumwambia kwamba mpenzi wake amerudi
Lakini msichana alichofanya ni kumsisitiza rafiki yake kwamba asimwambie yule kijana habari yoyote kuhusu yeye wala kile kilicho mtokea.
Tangu hapo kukawa kimya na hakupata kusikia habar yoyote kuhusu yule kijana.
Mpaka mwaka mmoja baadae alipokuja tena yule rafiki yake akiwa ameleta KADI YA MWALIKO KWAAJILI YA HARUSI YA KIJANA.
Msichana alipata mshituko mkubwa baada ya kufungua na kukuta jina lake ndani ya kadi hiyo.
Akiwa kwenye harakati za kutaka kumuuliza rafiki yake "nini kinaendelea"
Ghafla akamwona kijana akiwa amesimama mbele yake.
Kijana akatumia lugha ya ishara kumwambia "nimetumia mwaka mzima kujifunza lugha ya ishara ili niweze kuwasiliana na ww na kukufanya ujue kwamba sijasahau kuhusu ahadi yetu, Naomba unipe nafasi ili niwe sauti yako"
"Nakupenda sana"
--------------------------------------------------------------------
Siku chache baadae wapenzi hawa walifunga ndoa.
Hivi sasa Wanaishi kwa amani na furaha na Mungu amewabariki na watoto wawili.
MWISHO nami nakuombea kwa Mungu kile kilichopangwa kuwa chako siku zote kikawe chako. Chako peke yako.
Endelea kuwa na matumaini na Mungu wako, nae atakufanyia yale yaliyo mema kwako

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPATA MCHUMBA SAHIHI

TAMBUA UTAMU WA MAPENZI NA JINSI YA KUULINDA KATIKA MAHUSIANO

YAFAHAMU MAMBO YATAKAYO FANYA MAHUSIANO AU NDOA YAKO KUDUMU