YAFAHAMU MAMBO YATAKAYO FANYA MAHUSIANO AU NDOA YAKO KUDUMU
Katika maisha yoyote ya ndoa au mahusiano zipo changamoto mbalimbali
zinazo sababisha ndoa au mahusiano mengi kufa. Hata hivyo kufa kwa ndoa
nyingi na mahusiano hayo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu
wengi wamekuwa hawavitilii maanani .
Katika makala hii ya leo ningependa kushiriki pamoja katika kukuletea mambo mbalimbali yanayoweza kufanya ndoa au mahusiano yako yadumu . Mambo hayo ni pamoja na ;
👉Hofu
ya Mungu . Hakuna ndoa yoyote ile iliyoweza kuwa imara na kudumu ikiwa
hakuna hofu ya Mungu baina ya wanandoa . Kama ni kijana mwenye lengo la
kuingia kwenye ndoa yakupasa kujilidhisha juu ya mchumba uliyenaye kama
ni kweli ana hofu ya Mungu . Starehe ya muda mfupi isikufanye ukajisahau
na kuingia kwenye ndoa kwa kukurupuka .
👉Mapenzi
ya kweli baina ya wapenzi . Ili uweze kudumu katika ndoa au mahusiano
yoyote yale , yakupasa kuwa na mapenzi ya dhani kati ya wewe na mwenzi
wako . Kutokuwa na mapenzi ya kweli katika mahusiano hudharisha
udanganyifu mkubwa na usaliti . Mwisho wa udanganyifu huu ni kupungua
kwa mapenzi na hatimaye kuvunjika kwa ndoa au uchumba.
👉
Uvumilivu kwa mwenzi wako . Moja ya kitu kikubwa sanaa ambacho wengi
wetu tunaokuwa katika mahusiano au ndoa ni pamoja na kukosa uvumilivu.
Hakuna mahusiano yoyote yanayoweza kudumu pasipo kuwepo na uvumilivu
baina yenu . Tumekuwa wepesi kuchukua maamuzi zinapotokea sababu kadha
wa kadha hususani kutokuelewana . Ukijaribu kuchunguza yote hayo
utagundua kuwa yamepelekewa na wenzi kutokuwa na uvumilivu katika
mahusiano yao .
👉Uwezo
wa kujishusha . Jambo hili haswa kwa kiasi kikubwa lipo kwa sisi
wanaume . Imefikia hatua tunakuwa tumekosea wenzi wetu lakini hatuna
kasumba ya kujishusha . Moja ya nguzo imara inayoweza kusaidia kwa kiasi
kikubwa kudumisha mahusiano yenu ni pamoja na kila mmoja wenu kuthamini
uwepo wa mwenzake na kujishusha pale anapoona kuwa amekosea . Kufanya
hivyo kutaepuka kutumia muda mrefu kutatua ugomvi usio kuwa na msingi .
👉Hali
ya kuishi kwa kuthaminiana . Utu ni kitu muhimu zaidi katika mahusiano .
Endapo mahusiano yenu au ndoa yenu itapoteza hali ya utu basi itavuruga
mfumo mzima na mwenendo wenu . Katika mapenzi kila mmoja anawajibu wa
kujali na kuthamini utu wa mwenzake .
👉
Hali ya kujengeana misingi imara ya mapenzi mapema . Mahusiano yoyote
hudumu ikiwa wapenzi hao wamejengeana misingi iliyoimara katika
mahusiano yao. Misingi hiyo iambatane sambamba na kuelezana ukweli pindi
unapoona mwenzako haendi sawa . Kuwekana wazi mapema juu ya tabia
mnazoona kwenu ni chukizo .
👉Kujengeana
mipango thabiti juu ya matumizi ya pesa . Hakuna mahusiano yaliyoweza
kustawi ikiwa yanaendeshwa pasipo kuwa na mipango thabiti juu ya pesa
mnayoingiza . Wanaume wengi huchukia na hata wengine kutokusema wazi
pale wanapoona wanawake wao wamezidisha matumizi zaidi ya kipato chao .
Mnapokuwa katika mahusiano au ndoa ni wajibu wa kilammoja wenu
kuheshimu kipato mnachokipa ikiwa ni pamoja na kuweka mipango madhubuti
juu ya namna ya kuziendesha .
Mwisho , Tuheshim ndoa na mahusiano tuliyonayo katika kujenga familia na vizazi vilivyo bora katika maisha yetu .
Katika makala hii ya leo ningependa kushiriki pamoja katika kukuletea mambo mbalimbali yanayoweza kufanya ndoa au mahusiano yako yadumu . Mambo hayo ni pamoja na ;







Mwisho , Tuheshim ndoa na mahusiano tuliyonayo katika kujenga familia na vizazi vilivyo bora katika maisha yetu .
Comments
Post a Comment