Posts

JINSI YA KUPATA MCHUMBA SAHIHI

Moja ya mambo ya msingi ambayo kila kijana anahitaji ni Ndoa ya Kudumu ukiacha ongezeko la kufeli kwa ndoa nyingi. Wakati huohuo moja ya uamuzi (wa maana sana katika maisha ya binadamu ni kuamua nani atakuwa mume wako au mke wako na huu uamuzi ndiyo utakufanya uweze kuishi maisha ya namna gani katika ndoa yako na pia kuathiri kabisa mfumo wa maisha yako kuwa raha au kuwa karaha Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao. Huu ni ujinga muhusika mara nyingi ni wewe kwani asilimia 99 ni jinsi ulivyompata huyo mtu ambaye amesababisha ndoa yako au uhusiano kuvunjika. Mtu anayestahili kupewa lawama zote ni wewe. Kama hujaolewa au ndio upo kwenye process za kuolewa au kuoa,Fahamu kwamba hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha hapa duniani. Unahitaji kutumia akili zako zote, maombi yako yote, uw...

KWANINI UKATE TAMAA??

Kuna baadhi ya wanandoa tena kwa machozi wamekuwa wakilalamika kwamba partners wao hawawezi kuongea nao tena! Hawezi kushirikisha kitu chochote ingawa wanaishi nyumba moja, wanakula chakula kimoja, wanalala kitanda kimoja na wengine wana watoto pamoja. Wamejikuta ndoto zao zinayeyuka na ladha ya ndoa na maisha kwa ujumla imekuwa chungu. Kama unapitia upweke wa aina hii na kujikuta unajuta kuishi na mume au mke wa aina hii bado kuna matumaini na kuna nafasi kubwa ya kuweza kurudisha kwenye mstari, jaribu kufanya yafuatayo. 1;TEMBEA KATIKA ROHO. Ndoa si two-way street kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke au kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume bali ni three way street kati ya mke, mume na Mungu. Tunapotembea katika Roho, Mungu anamwaga upendo wa kutosha kati ya mke na mume. Breakdown yoyote kati ya mke au mume na Mungu huweza kusababisha wanandoa kuanza kuvurugana ndiyo maana wanandoa ambao hofu ya Mungu, kutembea katika Roho ni Nambari one basi wamebarikiwa kw...

USIJARIBU KUMFANANISHA NA WENGINE.

Kuna wakati huwa inashangaza sana ukisikia yale wanandoa wanafanya au wanataka yafanyike katika ndoa zao. Kama ni mwanamke basi una marafiki wanawake wenzako ambao waume zao inawezekana wana pesa nyingi kuliko mumeo, wamesoma kuliko mumeo, wana mali kuliko mumeo, wana akili kuliko mumeo, wanakuwa na muda zaidi na familia zao kuliko mumeo, wakivaa wanapendeza kuliko mumeo na pia wanabembeleza wake zao kuliko mumeo, au wana tabia njema kuliko mumeo au kama wewe ni mwanaume nawe una marafiki wa kiume ambao wake zao wapo hivyo. Je, ni mara ngapi umemlalamikia mumeo au mkeo kwa kumlinganisha na wanaume wengine au wanawake wengine? Inawezekana umemlalamikia mumeo au mkeo kwamba “Mwenzako jerry amepunguza uzito wewe umebaki umenenepeana kama kitimoto kwa nini? “Mwenzako George amenunua gari wewe nini kinakushida , wewe ni mwanaume gani?” “Mwenzako mama Noel kila siku ukienda kwake nyumba safi wewe inakuwaje chafu namna hii” Kama ni wewe utajisikiaje? Hapa msipotoana ngeu au k...

KUACHANA SI SULUHISHO.

Wewe ambaye umeoa au kuolewa na upo unafikiria kuachana na mwenzi wako. Fikiria upya uamuzi wako. Fikiria hao watoto mlionao, Fikiria nyakati zote nzuri mlizokuwa nazo pamoja kama mke na mume, Fikiria sehemu tofauti ambazo mlitembelea pamoja, marafiki wazuri mliokuwa nao wote wawili kama mke na mume. Iepuke talaka kwa gharama zote, sababu zinazokufanya uamue kuachana na huyo mume wako au mke wako zinaweza kuwa ndizo zitakazokuwa sababu mara nyingine tena mbele ya safari kama utaamua kuoa au kuolewa tena. Sasa unaachana na Jimmy kwa kuwa umechoka na tabia zake za kulewa sana pombe, au kukutaka sex mara nne kwa siku na next time unaweza kujikuta unaachana na John kwa kuwa anakupiga mingumi usiku kucha na yeye sex kwa mwaka mara moja. Inawezekana unataka kuachana na mary kwa sababu ni msumbufu na anakusema hata kwa vitu vidogo, hata hivyo unaweza kujikuta unaacha na Joyce baadae kwa sababu si mwaminifu katika fedha. Sasa utaishia wapi na hiyo project ya kuachana na kil...

MAMBO HUBADILIKA MKISHAOANA NA KUANZA KUISHI PAMOJA

Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja. Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanz a kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena. Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja. Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa. Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenz...

NI MAKOSA KUMPA MCHUMBA HUDUMA ZA MKE/MUME

Kawaida huwezi kumpa kila mwanaume huduma za mume wakati bado ni mchumba tu. Vijana wengi leo wanapochumbiana au kutafuta urafiki wa kawaida kati ya kaka na dada (dating) wengi hawajajua kwamba hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa na ni kama usaili tu wa kumpata mtu wa kuoana naye. Ndoa na uchumba (girlfriend/boyfriend) ni vitu viwili tofauti kabisa uchumba huhusisha kumfahamu mwenzako kama anafaa kuwa mke au mume na ndoa ni agano na kumkubali mtu kuishi naye “ hadi kifo. Hata siku moja uchumba si ndoa na ndoa si uchumba. Ukimpa mchumba haki za mume au mke siku mkiachana na huo uchumba (kitu ambacho ni kawaida kama ukiona candidate uliyenae katika uchumba hawezi kwa excellent material ya ndoa) utaumizwa zaidi hasa mwanamke kwani mwanaume anaweza kumpata binti mwingine jioni yake au usiku huohuo na akaendelea na maisha. Kinachoshangaza pia ni kwamba hata relationship inapovunjika mara nyingi mwanaume huumia kidogo kwa kuwa mwanaume siku zote anapoingia kwenye mapenzi hu...

MWANAMKE JIFUNZE HAYA

1. Ukiwa Kama mwanamke, pale panapotokea maudhi dhidi ya mpenzi wako, nyamaza kimya, ukimya wa mwanamke humsumbua akili mwanaume. Atahisi kuna jambo fulani kichwani mwako na kama anabusara atatafuta njia ya kusuruhisha. Usiwe mtu wa tit-for-tat. 2. Kama atakutumia ujumbe wa maudhi katika simu, usimjibu kwa maneno ya kuudhi pia. Muandikie "Samahani" au "Asante sana." 3. Hakuna mwanaume anapenda mwanamke anaemrudishia maneno, kama wewe ni mke uliye na busara, funga mdomo wako. Pale atakapokuwa ametulia ongea nae mmalize mgogoro. 4 Usilingie uzuri wako. Hujawaona wanawake wazuri wengi tu bado wako single, lakini wanaishia kuwa wezi wa waume za watu na uzuri wao kama wameshushwa toka mbinguni? Tabia yako itakuhifadhi katika moyo wake. 5. Kamwe usimfananishe na EX wako au mwanaume mwingine, huwezi jua huyo mwanaume nae ana mapungufu gani katika mahusiano yake. Binadamu hatuko 'perfect' 6. Usiwe wa kupokea tu, mnunulie chochote, haijalishi kama...